JIJI la Mwanza jana lilikumbwa na machafuko baada ya machinga kufanya vurugu na kuandamana wakipinga kuondolewa kufanya biashara katika maeneo ya mjini kati. Vurugu hizo zilisababisha kufungwa kwa maduka katika maeneo mbalimbali mjini hapa, kuvunjwa vioo vya magari, maduka na baadhi ya barabara kutopitika kwa muda huku kituo kidogo cha Polisi Pamba, kikinusurika kuvamiwa na kuchomwa moto.
Pichani mkuu wa mkoa wa Mwanza Abassi Kandoro akiwa na wana usalama;