Imekuwa ni kasumba kuwa tunasubiri mpaka mtu afe kwanza ndio tunaanza kummiminia sifa kedekede.Hii tabia siipendi sijui kwanini!! Pichani wachezaji mashuhuri enzi zao,kuanzia kushoto aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Argentina Diego Maradona  na kupata bahati ya kuifundisha timu ya taifa hilohilo kwenye kombe la dunia mwaka 2010 South Africa,Aliyesimama katikati mpaka leo hii anajulikana kama Mfalme wa Soka Duniani PELE wa Brazil,Pele alifahamika na kila mmoja enzi hizo kwa jinsi ya kupiga watu chenga na kufunga magoli ya ajabu akiwa uwanjani.Na huyu wa kulia pichani aliyevalia fulana ya kubana ni Zinedine Zidanne raia wa Ufaranza mwenye asili ya Afrika toka pande za Algeria,na huyu kwa kweli kwenye Soka aliheshimika sana miaka ya hivi karibuni kwa ustadi wake wa mpira bora.Kwa upande wangu nawapongeza sana kwa heshima walizonazo juu ya Soka.Mungu awaongezee umri mrefu na Afya njema,kwa kweli walitumika vyema katika Soka.