Kama utabahatika siku moja kuwaona kwa macho yako Wakimbizi nafikiri utatokwa na machozi.Huwezi kuamini endapo watakwambia tumetembea kwa miguu mwezi mzima mpaka kufika hapa tulipo na hatujui tunakwenda wapi!!Nchi yangu changa,naomba tusitake makubwa kwani sisi ni wachanga.Tusiige ya wenzetu,mbona yetu yanatuendea japo ni taratibuuu?Tujikune tunapofikia sio lazima kuwafuata wenzetu.
Angalia wenzetu Somalia,Sudan wanavyopata tabu na dhiki za maisha!!!tujitahidi kuilinda Amani yetu.