Simbaaa,Simbaaa,Simbaaa,Simbaa,Simbaaa,Pichani washabiki wa Simba Club wakishangilia ushindi walioupata jana dhidi ya Yanga Africans hukoo kisiwani Zanzibar katika kusheherekea sikukuu ya Mapinduzi.
 Kikosi kamili cha timu ya Simba Sports Club ambacho jana kilifanya vyema baada ya kuifunga timu ya Yanga mjini Unguja.Simba ilishinda goli 2 - 0 na Kutwaa kombe la  Mapinduzi.Pichani Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh: Dr Ali Mohamed Shein akipata picha pamoja na timu ya Simaba kabla ya Mpambano.
 Hiki ndicho kikosi cha Dar es Salaam Young Africa ambacho kilishindwa kufurukuta jana katika mashindano ya kombe la Mapinduzi hukoo Zanzibar na kuifanya timu ya Simba kutwaa ubingwa wa kombe hilo kwa ushindi wa bao 2 - 0.Pichani katikati aliyevalia suti ni Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh:Ali Mohamed Shein akipata picha na wachezaji wa Yanga kabla ya mpambano.
 Moja ya hekaheka katika siku ya mchezo hapo jana amabpo vijana walicheza soka safi na kila mmoja aliburudika.
 Wachezaji wa Simba wakishangilia bao lao walilolipata baada ya Mussa Hassan `Mgosi` Kuachia mkwaju uliojaa kimiyani.
Pichani Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr Ali Mohamed Shein akimkabidhi nahodha wa Simba Nicco Nyagawa Kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga timu ya Yanga kwa jumla ya mabao 2 - 0,mchezo uliofanyika katika uwanja wa Amani Zanzibar.