Mbelgiji na raisi wa Baraza la Umoja wa Ulaya bwana Herman Van Rompuys juzi alitangaza rasmi kuwa baada ya kukaa kikao cha pamoja na viongozi wakuu wenzake wamefikia muafaka juu ya matumizi ya pesa ya Euro.Lengo ni makubaliano juu ya miakakati ya mikataba ya makubaliano ya kuendeleza nguvu za utaratibu wa sera za kiuchumi.Amesema lengo ni kuboresha  ushindani na kupunguza mapungufu ya jumla yanayowakabili.