Tarehe 12 mwezi huu siku ya Jumamosi kulikuwa na Oparesheni maalumu ndani ya treni za Belgium,walikamatwa zaidi ya watu 10 ambao walikuwa wakisafirisha madawa ya kulevya aina ya Cocaine na baadhi ya watu walikamatwa na kilevi aina ya Bangi.Msako huo ambao uliendelea kwa siku nzima pia ulihusisha raia ambao wanaishi nchini kinyume na sheria, pia walikamatwa watu wengi sana.Hatua za awali zinasema watu wote walifikishwa kituo maalumu tayari kwa kufunguliwa mashitaka.