Hapo dawa ikiwa kweny masufuria inachemka ili wagonjwa wapatiwe tiba na babu.
Moto umekolea haswaa na dawa ndio inaiva vizuri hapoo,yani babu kwakweli kazi yake mmmh.
Akikwambia kwamba haka ndio kamti ambako anakatumia kama dawa ya kuponya watu magonjwa sugu huwezi amini.
Kwa kuwa wateja(wagonjwa) ni wengi dawa zinachemshwa kwa wingi na kuhifadhiwa kwenye ndoo za plastic.
Huko ni Landrover na Landcruiser tu kama una ka'baloon kako umeumia.
Baadhi ya gari ukwama kwa jinsi njia ilipokuwa full na kuharibiwa na wingi wa magari hayo.
Wanaochoka kukaa kwenye magari ujipumzisha pembeni mwa miti kwa kusubiria foleni ambayo haielezeki.
Kwa kweli babu kajua kuwapata wateja.foleni haziendi kabisaa na watu wanasubiri mpaka kufikia wiki mbili na zaidi.
Babu yupo makini katika kupima dawa yake,hapo anatoa Dozi na masharti yake.
Jamani huyu mtu hapa kafa ?mmmh nahisi baridi ya harusha inampata tabu kiduchu.
Baadhi ya watu maarufu nao walikuwepo kupata tiba ya kwa babu wa Loliondo.
Gari jinsi zilivyojaza watu huwezi hata kuamnini ni jinsi gani watu wanavyoumwa.
Taswira hii nimeipenda sana,babu katengeneza jina hasaa..kila anaekwenda urudi na matumaini.