Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uhandisi wa Barabara ya CGI, Radisay Ilic (kulia) akivuta maji kutoka kwenye moja ya visima vitano vilivyojengwa na kukarabatiwa chini ya ufadhili wa kampuni hiyo, mwishoni mwa wiki kwa wananchi wa Vijiji vya Kata ya Melela, wilayani Mvomero, Morogoro ambapo Mkuu wa Wilaya hiyo, Fatma Mwassa (hayupo pichani) alikabidhiwa visima hivyo kwa niaba ya wananchi wa kata hiyo.