Rais wa zamani wa chama cha Olimpiki nchini Uganda, Meja Jenerali Francis Nyangweso, alizikwa siku ya Jumamosi, 26 Februari 2011, nyumbani kwake Sofia, Busia, mpakani kati ya Uganda na Kenya. 
Alizikwa kwa heshima zote za kijeshi, zilizoendeshwa na wanajeshi wa Uganda wa UPDF.