Kuna baadhi ya magari hukwama njiani pindi yanapoharibika,pichani Landrover amabyo inasubiri Spare toka Arusha mjini zije zifungwe ili waendelee na safari,huku mabasi yenye shehena za watu yakisonga kwa babu Loliondo.
 Njia sio mbaya sana ila kuna vumbi sana,uenda wakati unakwenda kwa babu na ugonjwa huu na mwingine wa kifua ukakukumba njiani kwa jinsi ya vumbi lilivyokuwa jingi.
Ni hekaheka zisizokwisha wakati wa dozi ikiendelea,watu huwa wanakosa utulivu pale anapoona mgonjwa wake kazidiwa na kikombe kinachelewa kuwekwa dawa,uamua kumuomba babu kwa haraka ili kuokoa maisha ya mgonjwa wake.pichani ni hekaheka kama ujioneavyo. 
 Wakati babu anaendelea kutoa dozi na baadhi ya watu kuikubali dozi ya babu,wafanyabiashara wengi wamekuwa wakitumia jina la babu kama kigezo cha uchochezi wa maambukizi ya maradhi kisa dawa ipo,angalia hilo tangazo hapo juu kisha utajua nini lengo la mwandishi huyo.
Wagonjwa mbalimbali wanamiminika Loliondo kwa babu kwa ajili ya matibabu,pichani kuna wagonjwa wanaopelekwa wakiwa hoi bin taabani,ila kila mmoja huwa ajali kumpisha mwenziwe kwa kuwa ameshakaa pale takribani wiki tatu.pichani baadhi ya wagonjwa waliokuwa hoi.
 Maji ya kuchemshia dawa sio ya bomba wajameni,kivumbi kinakuja hata kama wewe ulikuwa tajiri vipi utakunywa tu hayo maji.pichani baadhi ya wasaidizi wa babu wakichota maji ili kuleta tayari kwa kuchemshia dawa.
 Dozi inaendelea kila mgonjwa anatapatiwa kikombe cha dawa,dau ni lilelile halipandi 500/=.
Sio watanzani tu wanaokwenda kwa babu,ni mataifa mbalimbali yanayokwenda kupata tiba hukoo Loliondo,pichani kama ujioneavyo mama wa Kihindi akimsalimia babu kwa heshima zote ili kupata tiba.
 Baada ya kutoa dozi ya kikombe babu anamtakia kila la heri kwa dua mgonjwa wake.
 Kwa kuwa watu ni wengi sana,hakuna nyumba za wageni za kuwalaza watu woote hao,kuna baadhi ya tents(mahema)yaliyofungwa kwa baadhi ya watu kijijini kule.
Sio usiku wala mchana utashangaa kuona watu wakiwa wamejilaza mahala popote.Hali ya watu kuwa wengi bado haijapungua kabisaa kijijini hapo kwa babu Loliondo.