Kulikuwa na burudani ya pekee ukumbini hapo,kila aliyetoa kiingilio chake alitoka na kusema hajaliwa na pesa yake imekwenda kihalali,Pichani kijana Diamond mbele na kushoto Ali Kiba na huku kulia ni Banana Zoro wakiwajibika kisawasawa kuwapa wananchi burudani.
Hapo ndugu Mpoki akionyesha Tuzo yake aliyoinyakuwa kutokana na wimbo wake wa Shangazi.Kiukweli watu wengi walisataajabu kwa kusikia Mpoki kapokea Tuzo hiyo kwani huyu ni mcheshaji mzuri,hawakutaraji kama angekaa chini na kutunga nyimbo nzuri kama hiyo.Hongera ndugu mpoki kwa kupokea tuzo hiyo.(picha kwa hisani ya Gsengo).