Rais Jakaya Kikwete amefanya uteuzi na kuwapandisha vyeo Maofisa waandamizi 21 wa Jeshi la Magereza.
Katika uteuzi huo, Rais Kikwete amemteua DCP Lucas Mwakalinga kuongoza Divisheni ya Huduma za Urekebishaji ndani ya Jeshi la Magereza.
Kamishina wa Magereza nchini, Augustino Nanyaro jana aliwavisha vyeo maofisa hao kwa niaba ya Rais Kikwete.(pichani ni kamishina wa magereza nchini afande Augustino Nanyaro)


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Magereza, Maofisa hao ni Lucas Mwakalinga ambaye anasimamia Divisheni ya Huduma na Urekebishaji, Naibu Kamishina (SACP) Erica Pesha aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa jeshi hilo mkoani Shinyanga na Naibu Kamishina wa Magereza (SACP) Chiza Ruvugo ambaye amekuwa Mkuu wa Magereza mkoani Arusha.
Waliopandishwa vyeo na kuwa Kamishna msaidizi mwandamizi wa Magereza ni SACP Mughenyi Omari (ACP) ambaye amekuwa Mkuu wa Magereza mkoa wa Pwani; SACP Cleophace Rweye (ACP) anayeongoza mkoa wa Dar es Salaam; SACP Miriam Mtambalike (ACP) amekuwa Mkuu wa Kitengo cha cha Huduma za Ustawishaji kwa wafungwa; ACP Yusuf Kimanji (ACP) anaongoza mkoa wa Kagera; SACP Nelson Sanawa (ACP) Mkuu wa Kitengo cha Mahabusu makao makuu; SACP Deusdedit Kamugisha (ACP) amekuwa Mkuu wa Chuo cha Udereva na Ufundi; SACP Anthonio Kilumbi (ACP) ameteuliwa kuwa mhandisi ujenzi wa Magereza Mkoa wa Iringa na SACP Agatha Kombe (ACP) amekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Singida.
Wengine ni SACP Stanford Ntirindula (ACP) amekuwa Mkuu wa Chuo cha Magereza Mbeya; SACP Edward Kaluvya (ACP) Mkuu wa Magereza Iringa; SACP Mtiga Omari (ACP) Mkuu wa kitengo cha Intelijensia Magereza makao makuu; SACP Raphael Molleli (ACP) Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mwanza na SACP Kibwana Kamtande (ACP) Mkuu wa Magereza mkoa wa Dodoma.
Maofisa wengine walioteuliwa ni pamoja na SACP Maecel Lori (ACP) aliyekuwa Mkuu wa utawala Arusha, SACP Gaston Sanga (ACP) ameteuliwa kuongoza Kitengo cha Ukaguzi wa Magereza makao makuu na SACP Mlasan Kimaro (ACP) Mkuu wa Gereza la kilimo Songwe mkoani Mbeya.