Hali katika mpaka wa Libya na Tunisia imekuwa mbaya zaidi huku maelfu ya watu kutoka ng'ambo wakiikimbia nchi hiyo.Waandishi wa habari walisema kuwa wafanyakazi wa kutoa msaada wameshindwa kuidhibiti hali hiyo kutokana na idadi kubwa zaidi ya wakimbizi wanaokimbia ghasia nchini humo.
Watu wapatao 140,000 wamezikimbilia nchi za Misri na Tunisia.
Kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi amesema kuwa anapendwa na watu wake wote, na amekanusha kuwa kuna maandamano yanafanyika mjini Tripoli.