Timu inayoongoza ligi kuu ya Uingereza Manchester United jana kwenye klabu bingwa barani ulaya iliweza kuuchezea vyema uwanja wake wa nyumbani pale ilipoiadhibu timu ya Marsseille toka nchini Ufaransa kwa magoli 2- 1.Ikicheza kwa nguvu zote na kushangiliwa na umati wa washabiki wa Old Trafford,waliweza kuwamudu vyema wapinzani wao.mpaka kipindi cha kwanza kinakwisha Manchester walikuwa mbele kwa goli moja.kipindi cha pili kilianza kwa kasi kila timu ikiwa makini zaidi,Manchester United waliweza kupata goli la pili katika dakika ya 75 na mfungaji akiwa yule wa goli la kwanza Hernandez,hata hivyo vijana wa Marseille waliweza kufuta machozi kwa kujipatia bao moja katika dakika ya 82 baada mchezaji wa Manchester West Brown kujifunga mwenyewe mpaka mwisho wa mchezo Manchester United 2 - 1 Masseille.