Ajali kubwa imetokea jumamosi hii katika jiji la Antwerpen nchini Belgium,Moto mkali uliokuwa unawaka chini ya Ardhi katika usafiri wa tram(trein ziendazo kwa kasi chini ya ardhi)Kikosi cha zima moto na polisi pamoja na raia wema walijikusanya kwa haraka katika kuuzima moto huo.hata hivyo chanzo cha moto huo bado hakijajulikana kutokana na hali ya moshi kuwa ni mkubwa sana na kufanya hata watu washindwe kuonana vyema.Pichani juu ni kituo kikubwa cha treni cha Antwerpen Centraal na chini ni kikosi cha zima moto kikiwahi kuuzima moto huo.
Kikosi cha zima moto kikiwa kazini kuuzima moto huo uliowaka ghafla chini ya ardhi.