Aliyekuwa mkurugenzi wa hospitali ameamuriwa kulipa paundi 25,000 kwa mwanammke mmoja wa Kiafrika ambaye amemweka kama mtumwa mjini London.
Mkurugenzi huyo alimweka kifungoni raia mmoja wa Tanzania kama mtumwa kwa miaka minne.
Wazee wa baraza walisikia jinsi Mwanahamisi Mruke alivyosafirishwa kwa ndege mwezi Oktoba 2006 na
kulazimishwa kufanya kazi saa kumi na nane kila siku kwa Bi Saeeda Khan ambaye ana umri wa miaka 68.
Mahakama ya Southcrown ilisikiliza namna ambavyo Bi Mruke aliye na umri wa miaka 47 alivyonyimwa haki ya kuwa na hati yake ya kusafiria na uhuru wake, na jinsi alivyohimili madhila aliyopata ili kumsomesha binti yake Afrika.
Khan alishtakiwa kwa biashara haramu ya kusafirisha mtu Uingereza na kumfanyisha kazi bila ujira wowote.
Bi Mruke alisema "hatomsamehe" aliyemweka kifungoni.
"Nilijihisi kama mjinga, nilifanywa kuwa mtumwa," Bi Mruke alisema.
Baada ya kumleta Uingereza kutoka Tanzania, Khan kutoka Harrow, kaskazini magharibi mwa London, mwanzo alimpa paundi 10 kila mwezi na kumfanyisha kazi mchana kutwa kila alipohitajika.
Hata hivyo baada ya mwaka mmoja akaacha kumlipa.
"Hata pesa nilizokuwa nimeahidiwa kulipwa sikupewa. Na nahisi vibaya kuhusu hili" Bi Mruke alisema.
"Nilikuwa nikitaraji kuwa nitalipwa mshahara na kuyaboresha maisha yangu. Lakini matumaini yangu yote yalipotea na nguvu zangu zilididimia na nikaanza kuumwa.