Kutana na mtoto mwenye umri wa miaka saba raia wa serbia anayefahamika kwa jina la Bogdan ambaye ameufanya ulimwengu kujiuliza kulikoni kutokana na uwezo wa mwili wake usio wa kawaida.Kulingana na taarifa za Shirika la habari la nchi hiyo mwili wa Borgan unanasa vyombo vya chuma kama vile vijiko, visu, uma, nyembe, funguo, misumari vyote katika hali ya kushangaza kabisa.

Wanasayansi wanaumiza vichwa, wasipate jibu la haraka kuwa hali hii ya mwili wa binadaamu ya kujitengenezea sumaku inatoka wapi? ni kama kiroja hivi! Na cha kushangaza zaidi hata sahani, vyombo vya kioo na hata kiendesha mbali ‘remote control’ vinanaswa na mwili wake, mama yyangu!!...
Baadhi ya vitu anavyovinasa vingine wala si vya vyuma kama vile glasi, alisema mwanahabari mmoja wa Serbia.