Maonyesho ya mavazi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni katika ukumbi wa Moven Pick Hotel katika kuchangia kina mama mambo ya uzazi salama.Pichani mwanadada mrembo kabisa akikatiza kwenye steji huku akishangiliwa na umati uliofika ukumbini hapo.
 Kazi za ubunifu zikiwa zinaendelea na huku watu kweli wakiwa wamependeza sana kama unavyojionea mwenyewe huyoo bidada hapo na nguo yake ya mtoko.
Utamu unakuja pale khanga inaponakishiwa vizuri na kuonekana na mvuto mzuri na wa kipekee,Kiukweli ubunifu wa mavazi kwa watu wa  nyumbani hivi sasa upo juu sana na unavutia.
Mbunifu wa kimataifa ambaye ni Mtanzania Mustafa Hassanali  akitoa shukrani kwa wageni waalikwa ambao walifanikisha harambee hiyo ya kuchangia fedha kwa ajili ya kina mama katika zoezi zima la uzazi salama.Onyesho la mavazi lilifanyika katika hotel ya Moven Pick jijini Dar es Salaam.