Raisi wa Marekani bwana Barack Obama amekuwa akipinga vikali viongozi wa Africa na kwengineko wanaong'ang'ania Madaraka kinguvu kiasi wanasababisha umwagaji wa damu katika nchi zao.
Raisi Obama amesema hayo pindi alipopokea malalamiko toka nchi mbalimbali duniani zikiwemo  Iran,Tunisia,Misri,Libya,Bahrain na Yemen.Akipokea malalamiko hayo kupitia vituo vya television na njia nyinginezo za mitandano bwana Obama ameombwa kutumia uwezo wake kupambana na viongozi hao wasiotakiwa madarakani.Raisi Obama ametangaza kushirikiana na wananchi hao vyema kuwaondosha madikteta wote kwenye nchi hizo zenye matatizo.