POLISI mjini Kahama mkoani Shinyanga wamemkamata Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, kwa tuhuma za kufanya mkutano usio halali na kinyume cha utaratibu katika mji mdogo wa Malampaka wilayani Maswa.