Sheria mpya ambazo zimetangazwa hivi karibuni juu ya wakimbizi walio na watoto wenye uraia wa Belgium hawatafukuzwa.Pichani ni baadhi ya watoto ambao wamezaliwa Belgium wakati bado wazazi wao wapo kwenye harakati za kuomba ukimbizi.Mahakama ya ulaya imebadilisha sheria mpya na kusema endapo watoto watazaliwa ndani ya nchi za ulaya na wao ni wanachama wa umoja wa ulaya kwa maana hiyo hakuna sababu za kuwafukuza wazazi wao.Kinachotakiwa ni wazazi wa watoto wao wafanye kazi ili kuweza kujimudu na familia zao.