Nick Cannon na mkewe Mariah Carey(Mwenye Ujauzito wa miezi 8) pichani wakitabasamu baada ya Nick kujieleza mbele ya umati wa watu kuhusu siku mkewe atakapojifungua mwanzoni mwa April mwaka huu."Ni ukweli usiopingika nafikiri nitazimia siku hiyo"Nick hakusita kujieleza kwa watu hisia zake kwamba anaogopa sana kuona mtu anapojifungua.Aliendelea kusema "Nimeomba wapenzi wangu na mashabiki wote wanipe japo mbinu siku hiyoo mke wangu akipata uchungu nianzie wapi"?"baadhi ya rafiki zangu wameanza kunipigia simu na kunitaka nisiwe na hofu siku ikifika nitaona na kujua cha kufanya"alimaliza.Maganga One Blog inapenda kumpa ujumbe bwana Nick kwamba "Ukiyavulia huna budi kuyaoga".