Ni sekeseke la haja langoni mwa timu ya taifa ya Afrika ya kati,ambapo wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania wakilishambulia lango hilo vilivyo.Timu ya Taifa ya Tanzania ilibamiza bila huruma tilu hiyo jwa jumla ya goli 2 - 1 na kuifanya Tanzania kuwa na matumaini makubwa ya kusonga mbele katika michuano hiyo.
Ushindi jamani ni raha sana,hapa ni timu yetu ya taifa ya Tanzania baada ya kupata bao la pili dakika ya 89 baada ya mchezaji Mbwana Sammata kuweka mpira kimiyani kwa kichwa safi na kufanya uwanja ulipuke kwa chereko na nderemo zisizo za kawaiadaMCHEZAJI Mbwana Samatta ametoa raha kwa Watanzania baada ya kuifungia timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars, bao la ushindi katika mechi dhidi ya Afrika ya Kati iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Mechi hiyo ni ya Kundi D katika harakati za kuwania kufuzu fainali za Mataifa Afrika zitakazofanyika mwakani Gabon na Equatorial Guinea.

Samatta alifunga bao hilo dakika ya 89 zikiwa ni dakika kama 25 hivi tangu ameingia uwanjani kuchukua nafasi ya Henri Joseph na kufunga bao hilo lililoifanya Stars iibuke na ushindi wa mabao 2-1.

Samatta alifunga bao hilo kwa kichwa baada ya kuunganisha vema mpira wa kona uliopigwa na Nurdin Bakari na mpira kwenda moja kwa moja kutikisa nyavu za Afrika ya Kati.

Kabla ya bao hilo, Samatta alikosa bao dakika ya 88 baada ya kuunganisha vibaya kwa kichwa mpira wa Mrisho Ngassa na hivyo bao alilofunga ni kama alifuta makosa yake.

Katika mechi hiyo, wageni ndio waliokuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza katika
dakika ya pili ya mchezo, lililofungwa na Mabide Vianney.

Bao hilo lilidumu mpaka mapumziko na dakika nne baada ya kuanza kwa kipindi cha pili Shaaban Nditi alifunga bao la kusawazisha baada ya kuunganisha pasi ya Ngassa.

Nditi alifunga bao hilo kwa ustadi, alipoupata mpira wa Ngassa hakuwa na papara kama walivyokuwa wakifanya wenzake mwanzo, aliutuliza na kupiga mpira uliokwenda moja kwa moja nyavuni.

Kwa ujumla, Stars ilitawala karibu sehemu kubwa ya mchezo lakini umaliziaji mbaya wa
washambuliaji wake uliikosesha mabao mengi.

Matokeo hayo yanaifanya Stars ilingane pointi na Jamhuri ya Kati, zote sasa zina pointi nne na ilikuwa ikisubiriwa mechi ya jana ya kundi lao kati ya Morocco na Algeria kuona nani ataongoza kundi hilo.

Kabla ya mechi hiyo, Morocco ilikuwa na pointi nne na Algeria ilikuwa na pointi moja, hivyo kama Morocco ingeshinda ingeongoza kundi kwa pointi saba na kama ingefungwa, timu zote nne za kundi hilo zingekuwa na pointi sawa.

Akizungumza baada ya mechi, Kocha wa Stars Jan Poulsen alisema anawashukuru wachezaji wake kwa kuibuka na ushindi katika mechi ya jana kwani Jamhuri ya Kati si timu mbaya.

“Kipindi cha kwanza hatukuwa makini, tulipoteza nafasi kama tatu za wazi, lakini kipindi cha pili tulibadilika na kupata mabao hayo, nawashukuru sana wachezaji wangu na kuwapongeza…
sasa siwezi kusema kitu nasubiri matokeo ya mechi ya Morocco na Algeria,” alisema.

Stars: Shaaban Kado, Shadrack Nsajigwa, Aggrey Morris, Nadir Haroub, Idrisa Rajabu/ Stephano Mwasika, Nurdin Bakari, Shaaban Nditi, Henry Joseph/ Mbwana Samatta, Mrisho Ngassa, Mohamed Banka, Athumani Machuppa/ John Bocco.

Afrika ya Kati: Lembet Geoffroy, Ozingoni Nicaise/Boutou Audin, Momi Hilaire, Enza Manase, Kette- Vouama Foxi, Manga David/Dopekoulouyen Charly, Kassai Fernander/Kemo Fernand Onassis, Salif Keita, Lignazi Romaric Freddy-A, Mabide Vianney, Anzite Franklin.