Balozi  Ombeni Sefue(Tanzania) amesema kuwa Somalia ni Tishio kubwa kwa Amani na usalama kwa bara la Afrika na ameendelea kusisitiza kuwa Somalia si tishio kwa bara la Afrika tu bali ni kwa dunia kwa ujumla.Tanzania inaunga mkono jumuiya ya Umoja wa mataifa kwa kuunda vikosi vya kuisaidia Somalia.Pichani ni Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Somalia bwana Mohamed Abdullahi Mohamed akizungumza wakati Baraza kuu la usalama likijadili hali ya siasa na machafuko nchini Somalia.Bwana Mohamed aliliomba baraza la usalama na vikosi vya usalama vya afrika kuisaidia nchi yake kupambana na kundi zima ka Al Shaabab amablo limekuwa tishio nchini humo.