Tunaposhauriwa kutunza mazingira ina maana tutunze kiukweli mazingira kila mahala,pichani kina mama na watoto wao wakimaliza shughuli zao za uchafuzi wa mazingira kwa njia mnazoziona,Watoto wanaoga,wao wanafua na kama mjuavyo watoto wanajisaidia kabisaa humohumo.Ng'ombe wanakunywa maji na kuyachafua kwa vinyesi vyao na hapohapo baadae wanayachota kwa shughuli za matumizi ya nyumbani,kitu ambacho ni hatari kwa afya za binadamu.