Badala ya kwenda shule wanaponda kokote ili wapate pesa za mahitaji ya familia zao.Ukiwaangalia kwa harakaharaka watoto wamezeeka kwa kazi ngumu ambayo haiendani na umri wao.Hiyo nyundo anayotumia kupondea kokote inafika hata kilo moja na nusu.Serikali isipochukua hatua nzuri kwa maendeleo ya watoto hapo baadae itakuwa tabu sana nchini.