Majeshi ya serikali ya Libya yanasogea kuelekea kwenye bandari ya mafuta ya Ras Lanuf, yakiwasukuma waasi upande wa magharibi.
Mji wa Bin Jawad, uliopo kilomita 50 kutoka Ras Lanuf, sasa unadhibitiwa na majeshi yanayomtii kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi.
Umoja wa Mataifa umemtaja aliyekuwa
waziri wa mambo ya nje wa Jordan kama mjumbe wake nchini Libya, ambapo waasi wanaompinga Gaddafi wakipambana katika wiki yao ya tatu.
Umoja huo pia ulisema, takriban watu 200,000 wamekimbia ghasia hizo.
Unatoa wito wa kutolewa dola za kimarekani milioni 162 ili kusaidia watu 600,000 wanaoishi ndani ya Libya watakaohitaji msaada wa kibinadamu, na pia watu 400,000 wanaoondoka nchini humo kwa muda.