SIKU moja baada ya Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) kupandisha nauli za usafiri wa daladala katika Jiji la Dar es Salaam, wananchi wameilalamikia hatua hiyo, huku wakitaka huduma zinazotolewa ziboreshwe kwanza.
 
Moja ya vitu vinavyopingwa na wananchi ni usafi wa makondakta,lugha chafu wanazotumia ndani ya daladala,kujaza watu kupita kiwango,kutotoa tiketi,usafi ndani ya gari,madereva kukatiza safari na ubora wa magari yao.Pichani juu abiria wakigombea daladala kitu ambacho wananchi hawakipendi,picha ya pili askali wa usalama barabarani akimkamata kondakta aliyekuwa akitoa lugha ngumu ndani ya basi.