Amri Mkuu wa Waanswari-Sunna na Wasalafia nchini, Sheikh Salumu Sima, amesema muandamo wa mwezi wa Shawwali (Mfungo Mosi), leo au kesho jioni.
Katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari jana jijini Dar es Salaam, Sheikh Sima alisema kwamba muandamo huo utategemea mwandamo wa Mwezi wa Kimataifa.
“Jijini Dar es Salaam, Sala itakuwa saa mbili asubuhi katika viwanja vya Jangwani, Mnazi Mmoja, Kidongo chekundu, Mburahati barafu, Mwembe Yanga/Mwembe Ladu na Mbagala Zakhiemu. Na mikoani, sala itakuwa katika viwanja vya wazi vya miaka yote,” alisema.