Kazi ilikuwapo ukumbini hapo,yani ni full Arambaa arambaa tena Haaaam haaaam
Wageni mbalimbali walifurika ukumbini kushuhudia mambo ya mzee Yusuf akiwapagawisha waliofika ukumbini hapo.
Waaww!!! mashostisho walipendeza sana,show ilipendeza sana na kila kitu kilikwenda sawasawa
Mzee Yusuf akiendeleza kuwapagawisha mashabiki wake jijini Den Haag.
Hapo mwenye kuramba aliramba kisawasawa,full kujiachia,full mzuka ndani ya Den Haag.
Maganga One kikosi kazi kilikuwepo kuhakikisha mambo yanakwenda sawasawa katika kuwaletea habari ndani ya blog.Maganga One Blog imetoa ajira kwa wake na wanaume sawasawa ili kuleta maendeleo katika jamii yetu
Full kujiachia,mashostisho kibaooo ukumbini,kwa mbali anaonekana bwana Kabila mwenye shati la mikono mirefu akiwa na mashabiki wengine wakishuhudia mambo ya kurambishwa yanavyoendelea.
Mfalme Mzee Yusuf akipata picha na makamanda wa Holland,aliyevalia kofia nyuma ni Brother Bachala mmoja wa watu waliofanikisha show ya mzee Yusuf kwenda hewani.
Mzee Yusuf mfalme wa Taarabu Tanzania alitoa zawadi kwa dada aliyependa ukumbini,hapa akimpongeza dada aliyevaa vazi la kiafrika japo yupo ulaya na ndiye mshindi aliyependeza siku hiyo ya jana.
Mashostisho wakiwa wamepozi wakifuatilia kwa makini nini knaendelea ukumbi hapo,yani full kupendeza.
 Haina shobo,haina Kwere wala haina kujiashua yani hapo ni full mzuka,bidada Vicky Promota wa kike aliyeweza kulisukuma Jahazi vyema na show kwenda hewani kama kawaa...
Mzee Yusuf alitoa zawadi kwa mtu aliyependeza ukumbini hapo na alitoa zawadi kwa mtu aliyeweza kucheza vizuri taarabu inavyotakiwa kuchezwa,Pichani ni Mama Sharon akipata picha ya pamoja na Mzee Yusuf mara baada ya kupokea zawadi yake ya mwanadada aliyeweza kucheza vizuri taarabu vile inavyotakiwa kucheza.
Mmoja wa Viongozi wa kampuni ya UWATU akimkabidhi AWARD  Mzee Yusuf kama heshima ya kuweza kufanikisha muziki wa Taarabu nchini Tanzania kukubalika.
Mzee Yusuf akiitazama vyema Award yake huku akitoa maneno ya shukrani kubwa sana kwa mambo mazuri ambayo aliyapata toka kwa wenyeji na waandaji wa show yake. 
Mzee Yusuf akipongezwa kwa zawadi yake ya Award ya  heshima kwa kuendeleza vyema muziki wa taarabu nchini Tanzania.Pichani akipata Flash na bidada mrembo kabisa jijini Den Haag.
Hapo kila mmoja bize kuangalia mambo ya mfalme Mzee Yusuf akipagawisha mashabiki. 
Mashostisho kushoto ni Bidada Vicky na Kulia ni bidada Amina hapo wakipata Flash kama kumbukumbu ya kukubaliana na Mfalme jinsi alivyowarambisha.
Acha nijimwaga mieee na Mpenzi wangu miee acha nijimwage mie na mpenzi wangu jamaaaaaaniii!!
Walioshindwa kujizuia kucheza na mfalme walicheza pamoja
Mashostisho kibaoo wakisubiri show kuanza.ilikuwa hapatoshi kwa shangwe.
Zuhra Biboze hakubaki nyuma pale alipokuwa karibu kabisa na Mzee Yusuf ili kupata kumbukumbu ukumbini hapo.
Bidada Amina alimwaga Euro ukumbini hapo,maana show ilimfurahisha vilivyo.
Mzee Yusuf akipata Flash na Maganga One Blogger.Tulipata muda wa kuongea na Mzee Yusuf na mahojiano yatawekwa kwenye ukurasa siku maalumu.
Bidada Amina akiwa na Euro 200 mkononi kwa ajili ya kumtunza Mzee Yusuf kwa jinsi alivyowarambisha kisawasawa.
Mzee Yusuf akiwa na mmoja wa Mapromota wa kike nchini Holland,bidada Vicky..Vicky ndiye aaliyeongoza shughuli za shughuli zote ukumbini hapo.
 Kila kinywaji kilipatikana ukumbini hapo,huduma ya nyama choma na madikodiko yani ilikuwa haina Majrotooooooooo. 
Alwatan James Biboze kushoto ambaye ukifika kitongoji cha Beverwijk na kuuliza yoyote atakuonyesha,Pichani akipata picha na wshiba wake Mzee Yusuf Mfalme.
Wageni mbalimbali toka mataifa mbalimbali wenye nyazifa mbalimbali walikuwepo ukumbini hapo.
Mzee Yusuf akipata picha na mashabiki wa muziki wake.
Mfalme wa Taarabu Tanzania,Mzee Yusuf akikonga nyoyo za wapenzi wake jijini Den Haag.
Kikosi kazi cha Maganga One kilipata picha baada ya uwajibikaji ukumbini,hapa Mzee Yusuf akila Snap na Maganga One Team.
Dj aliyekaranga vyombo ipasavyo na kumfanya Mzee Yusuf Kuwarambisha mashabiki kisawasawa,ni Dj Alein.Dj Alein ni Dj anayekubalika nchini Holland.