Nchi za Muungano wa Afrika zinazochangia wanajeshi wa kulinda amani nchini Somalia pamoja na wajumbe wa ukanda wa pembe ya Afrika wamekutana katika mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa kujadili mustakbala wa operesheni hiyo ya kulinda amani.
Pamoja masuale mengine yanaangaziwa ni uhaba wa fedha unaokabili operesheni hiyo.
Operesheni hiyo iliyodumu kwa miaka mitano sasa inahitaji wanajeshi zaidi, lakini hadi sasa ni Burundi na Uganda pekee ambazo zinahudumu nchini Somalia.
Lulit Kebede msemaji wa Muungano wa Afrika amesema mkutano huo wa Addis Ababa umewaleta pamoja mawaziri wa ulinzi wa Uganda, Burundi, Kenya Djibouti na Ethiopia kwa lengo la kujadili hali ya kisiasa, operesheni za kijeshi pamoja na mustakbala wa operesheni ya kulinda amani nchini Somalia.
Licha ya mkutano huo kuwa wa faragha, taarifa zinasema wajumbe hao pia walijadili azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo linaidhsinian vikosi hivyo kuendelea kuhudumu nchini Somalia hadi mwezi October mwaka wa 2012.
Mkutano huu unakuja wakati Kenya nayo imetuma majeshi yake nchini Somalia katika harakati za kupambana na kundi la Al-Shabab, baada ya utawala wa Nairobi kulihusisha kundi hilo na visa vua utekaji nyara wa wageni ndani ya ardhi ya Kenya.

Lakini suala lingine nyeti ambalo wajumbe hao wasingeweza kuliepuka kujadili ni ukosefu wa fedha ambao unadaiwa kutatiza operesheni nzima ya kijeshi ya Muungano wa Afrika nchini Somalia .
Maafisa waandamizi wa kijeshi wa operesheni ya AMISOM wamekiri kuwa wana pengo la dola millioni kumi, hali ambayo inakwamisha kupelekwa kwa wanajeshi wa ziada nchini Somalia, pamoja na kuendelea na vita dhidi ya kundi la Al-Shabab katika mji mkuu na maeneo mengine nchini.
Nchi za Djibouti na Sierra Leone ambazo kulingana na mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia balozi Augustine ahiga zilitarajiwa kutuma vikosi vyana Somalia kujiunga na operesheni ya AMSIOM, baado hazijatia taarifa kuhusu lini watajiunga na operesheni hiyo na huenda kuchelewa kwao kumesababishwa na hali hiyo ya ukosefu wa fedha.