Waziri wa habari nchini Equatorial Guinea amesema asili mia 99 ya wapiga kura wameunga mkono marekebisho ya katiba kupitia kura ya maoni. Waziri
Jeronimo Osa Osa Ecoro amemsema thuluthi tano za kura zimehesabiwa.

Upinzani umepuzilia kura hiyo ya maoni na kuitaja kama unafiki mkubwa. Marekebisho mapya ya katiba yamependekezwa na rais Teodoro Obiang Nguema ambaye amekuwa madarakani kwa miongo mitatu.

Miongoni mwa marekebisho ya katiba mpya ni pamoja na kupunguza mihula ya urais na kubuniwa kwa wadhifa wa Makamu wa Rais.