DIVA wa filamu za Kibongo, Irene Pancras Uwoya ‘mama Krish’ amefanywa ‘panchingi begi’ na muwewe, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ pale alipochezea kichapo ‘hevi’ baada ya kubambwa na ujumbe mfupi wa maneno’SMS’ kutoka kwa staa wa Bongo Fleva (jina tunalo).

Kwa mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo lilitokea maeneo ya Sinza Afrikasana jijini Dar es Salaam wiki iliyopita ambapo wawili hao wameweka maskani yao mapya pande hizo.

UWOYA ASHINDWA KUJITETEA
Ilidaiwa kuwa, Uwoya alichezea kichapo hicho baada ya kumpandisha hasira mumewe kwa kushindwa kujitetea kuhusu ujumbe huo wa kimapenzi na kumjibu jeuri Mnyarwanda huyo anayesakata soka la kulipwa nchini Cyprus pale alipomuhoji kuhusu uhusiano wake na staa huyo wa Bongo Fleva.

Kikifafanua zaidi, chanzo chetu kilisema kuwa ilikuwa usiku ambapo Uwoya na mumewe wakiwa sebuleni, ghafla simu ya mrembo huyo aneyetamba kwenye filamu ilitoa mlio kuashiria kwamba ujumbe mpya umeingia, ndipo mumewe alipoomba kuusoma kabla Uwoya hajautia machoni.

BABA KRISH ABADILIKA GHAFLA
“Baada ya baba Krish kuusoma ujumbe ule na kukutana na silabi za mapenzi, uso wake ulibadilika ghafla na alipomuuliza Uwoya akawa mbogo katika kumjibu mumewe,” kiliambaa na mistari chanzo chetu.
Hata hivyo, habari zilizidi kupasua ngoma za masikio ya ‘vuvuzela’ wetu kuwa, baada ya Uwoya kuwa mkali ikawa kama ametupa kijinga cha moto kwenye pipa la petroli, nyumba ilifuka moshi kwa Kataut kumvaa Uwoya kama mpira wa faulo na kuanza kumpa kisago bila simile.

MSIKIE UWOYA
Katika kuweka sawa mzani wa habari hii, paparazi wetu alimwendea hewani Uwoya ambaye alikiri kutokea kwa sintofahamu kati yake na mumewe ingawa alikana kubondwa:
“Mh…, aaah… eeeh mbona sijapigwaa, hebu jaribu kumpigia yeye (Kataut) uone atasemaje, ila ukweli ni kwamba tulikuwa na ugomvi wa mambo yetu ya ndani na umeisha.”

NI KWELI NDIKUMANA UMEMPIGA UWOYA?


Kwa upande wake Kataut alijitetea kuhusu suala hilo la kichumbani zaidi kwa kuachia senteni hizi:
“Ni kweli kabisa tulikuwa na ugomvi uliosababisha tukapishana kauli, lakini tumeshayamaliza, tunaishi kama kawaida.”
Ijumaa Wikienda: Lakini ni kweli ulinasa ujumbe wa wa mapenzi kwenye simu yake?

Kataut: “Aaah…, hapana ilaaa…ni mambo ya ndani ambayo siwezi kuyaweka hadharani kwa kuwa sasa tunaelewana vizuri na mke wangu.”
Uwoya alishawahi kunukuliwa na gazeti ndugu la hili, Risasi Jumamosi akisema kuwa tatizo mume wake ana wivu sana. Pia alidai kuwa mara nyingi Baba Krish amekuwa na utaratibu wa kukaa na simu yake.
NI STAA GANI WA BONGO FLEVA?
Hata hivyo, gazeti hili linaendelea kupeperuka angani kusaka jina la msanii huyo wa Bongo Fleva aliyeitia majaribuni ndoa ya Uwoya na uchunguzi ukikamilika, gazeti hili litaanika kila kitu.