Ofisi za jarida moja la vibonzo nchini Ufaransa, Charlie Hebdo, zimeteketezwa na watu wasiojulikana katika siku ambayo jarida hilo limechapisha kibonzo cha Mtume Muhammad katika ukurasa wake wa mbele.

Hata hivyo moto huo ulidhibitiwa haraka na hakuna aliyejeruhiwa.

Jarida hilo lilikuwa limechapisha makala maalum yaliyokejeli sheria za kiislamu maarufu kama Sharia na pia ufanisi wa makundi ya kiislamu nchini Tunisia na Libya.

Wasimamizi wa jarida hilo wamekanusha madai kuwa walidhamiria kuchokoza wafuasi wa dini ya kiislamu.

Mtandao wa jarida hilo ulivamia na kuandikwa maneno kwa lugha ya kiingereza na kituruki kulaani uamuzi wake wa kuchapisha kibonzo hicho cha Mtume Muhammad.