KATIKA harakati za kutafuta usawa wa kijinsia, mbunge ‘mwanamke wa shoka’ wa Jimbo la Kasarani nchini Kenya, Elizabeth Ongoro anadaiwa kumpa kipondo mumewe, Ferdinand Masha Ongoro hadi kupoteza fahamu.

Tukio hilo lilijiri hivi karibuni jijini Nairobi ambapo baada ya jamaa huyo kupokea kipigo ‘hevi’ alikimbizwa katika Hospitali ya Nairobi huku akiwa na maumivu makali sehemu ya kichwani kutokana na ngeu alizotolewa na mkewe.

Akizungumza kwa tabu hospitalini hapo na Gazeti la Star la nchini humo, mwanaume huyo ambaye ni mfanyabiashara mkubwa jijini Nairobi alisema:

“Tulikuwa nyumbani na mheshimiwa kama ilivyo desturi yetu, kulitokea kutoelewana kidogo, nashangaa kujikuta hapa hospitalini.
“Aaah! (akiona aibu) Ni ishu ndogo sana ya kifamilia, kwanza tuna watoto wadogo ‘so’ namshukuru Mungu nipo hai. Siwezi kueleza chanzo cha ugomvi. Nitafute siku nyingine.

Kwa mujibu wa wanaume waliofuatilia mkasa huo, kuna kila sababu ya kuanzisha chombo au taasisi ya kutetea wanaume wanaonyanyaswa na wake zao kwani idadi ni kubwa.