Step in...leo ndio leo Hakunaga ndani ya Utrecht nchini Holland.
Nimezunguuka mitaani na mwenyeji wangu mpaka nikaona mmh miguu inauma acha nijipumzishe kidogo.Nimejikalia kidogo ili kuangalia hali ya hewa mtaa wa Grote Markt na pilikapilika za watu utasema mtaa wa kongo Dar.
Nilipoliona hili gari hili likanikumbusha mbali sana,ukilingalia gari hili utasema ni gari bovu ila kumbe ni gari zima kabisaa.
Nimependa sana muonekanano wake kwa pande zote wa hili gari.Linaitwa Cetron,ni gari zuri sana ila lina gharama sana katika matunzo na spare zake.Usiku wa leo tutakuwa na Suma Lee nchini Holland,subirini mapicha na matukio yatakayojiri.