Kutokana na hatua ya kufunga barabara watu wamelazimika kutembea kwa miguu nao polisi wakipiga marufuku kusanyiko la aina yoyote kwenye eneo husika.

Toka angani eneo la mahakama ya wilaya Nyamagana.
Jumla ya watuhumiwa wanne wanadaiwa kushirikiana kuchoma Korani, asubuhi ya leo wamefikishwa mahakamani hapa kujibu mashtaka dhidi yao katika kesi inayotajwa kuahirishwa zaidi ya mara nne sasa kutokana na kuhofia usalama wa watuhumiwa.

Watuhumiwa wanaohusishwa na kesi hiyo ni waumini wa Kanisa la Tanzania Assembly of God (TAG) ni Tumaini Jumanne (30) ambaye ni mwalimu wa Biblia, Petro Mashauri (29) mfanyabiashara, Dickson Magai (30) mfanyabiashara na mwanamke pekee, Kalista Mlomo ambaye ni mkulima.

Wakikabiliwa na mashitaka matano ambayo ni kula njama, kufanya kusanyiko lisilo halali, kuingia kwa jinai nyumbani kwa Husna Hamis na kuharibu mali, pamoja na lile linalozungumzwa zaidi la kudhalilisha dini kwa kuchoma moto kitabu cha Korani Tukufu.

Askari wa jeshi la polisi wakifanya doria eneo la mahakama.

Katika hali isiyotarajiwa, ghafla mazingira ya mahakama ya mwanzo iliyoko karibu na ofisi za idara ya maji safi na maji taka jijini Mwanza, eneo la Kemondo na maeneo ya Ghandh hall, Polisi wamelazimika kulipua mabomu ya machozi majira ya saa nne asubuhi ili kuwatawanya waandamanaji waliofurika kwa wingi nje ya mahakama ya Wilaya ya Nyamagana wakifanya vurugu kushinikiza maamuzi yafanyike dhidi ya watuhumiwa wa kesi hiyo.

Si biashara tena bali msaada kukosha macho kwa maji ya kahawa.