Wapenzi wa muziki wa Bongoflava weekend hii watapata burudani ya aina yake katika kitongoji cha UTRECHT nchini Uholamzi,Akiongea kwa uhakika na kujiamini zaidi Suma Lee  ametamba kuwakonga wapenzi wa muziki nchini nchini hapa.

Akikata kimya cha muda mrefu bila kusikika Suma Lee ametoka na nyimbo mpya ambayo ni gumzo kila kona ndani na nje ya nchi...nyimbo inayokwenda kwa jina la ``HAKUNAGA``Ni msanii mkongwe mwenye uhakika na kazi zake.Amewataka wapenzi wake kujumuika pamoja nae siku ya jumamosi katika ukumbi Sport cafe de Dreef,Schooneggendreef 27,Utrecht.show itakuwa nzuri na kila mmoja ataburudika.Wapenzi wa Suma Lee mnaombwa kufika kwa wingi kupata ladha ya nyumbani ya muziki wa nyumbani..tusimalize uhondo hapa kwani kuna kila aina ya suprise ukumbini huko,njoo ujionee bila kukosa na ukilisoma tangazo hili mwambie na mwenzako ili muwe wote ukumbini.