YAH: SIKUKU YA EID EL HAJI
Tarehe 6 Julai 2011 Jumapili ni sikukuu ya Eid El Haji sawa na mwezi 10 Dhul Hijja 1432.


Kwa mujibu wa Kaimu Mufti wa Tanzania, Sheikh Muhidini Mkoyongore, Swala ya Eid Kitaifa itaswaliwa katika Masjid Al Farouq iliyoko BAKWATA Makao Makuu, kuanzia saa 1.30 asubuhi ikifuatiwa na Baraza la Eid.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inawatakia waumini wote wa dini ya Kiislam Eid njema na yenye upendo, amani na utuivu.