Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Akiwa Katika Picha Ya Pamoja Na Makamu Wa Rais Wa Shirika La Uwekezaji Vitega Uchumi Nchini Marekani (Opic) Bibi Mimi Alemayehou.Kushoto Ya Balozi Seif Ni Naibu Waziri Wa Afya Zanzibar Dk. Sira Ubwa Mamboya Na Kulia Ya Bibi Mimi Ni Waziri Wa Nchi Ofisi Ya Makamu Wa Kwanza Wa Rais Wa Zanzibar Mhe Fatma Fereji.

Waziri wachi ofisa ya makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Mh Fatma Alhabib Fereji akimfurahishia Makamu wa Rais wa shirika la Opic Bibi Alemayehou baada ya kumfalisha vazi rasmi la utamaduni wa Zanzibar. Kitendo hicho pia kilishuhudiwa na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.



Zanzibar imeshauriwa kulitumia vyema soko la Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Mashariki kwa lengo la kukuza uchumi wake na kuondokana na kutegemea zao moja la karafuu kama mhimili wa Taifa.

Ushauri huo umetolewa na Mkamu wa Rais wa Shirika la uwekezaji Vitega Uchumi la Kimataifa Nchini Marekani { OPIC } Bibi Mimi Alemahou wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Makao Makuu ya Shirika hilo Mjini Washington DC Nchini Marekani.

Bibi Mimi alimueleza Balozi Seif na ujumbe wake ulioko nchini Marekani kwa ziara ya Kikazi ya kuitangaza Zanzibar kwa wekezaji kuwekeza Zanzibar kwamba Shirika hilo tayari limeshaandaa mpango wa kuwekeza ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki likilenga kusaidia eneo hilo Kiuchumi.

Alisema mpango huo una nia pia ya kuijumuisha Sudan ambayo imekuwa ikikabiliwa na ukame wa mara kwa mara licha ya kwamba haimo ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki { EAC }.

“ Tumelenga zaidi kuisaidia Sekta Binafsi kwa vile jamii kubwa hasa ndani ya Bara la Afrika imekuwa ikikabiliwa na Uchumi duni ”. Alisema Bibi Mimi Alemayehou.



Bibi Mimi alifahamisha kwamba huduma za Shirika hilo la OPIC mara kahaa huelekezwa katika kutoa huduma za Kijamii kwenye sekta Binafsi kupitia Makampuni ya Kimarekani Chini ya Shirika la Misaada la Marekani US aid.



Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi ameuambia Uongozi wa Shirika hilo la Uwekezaji Vitega Uchumi la OPIC kwamba Zanzibar bado inaendelea kutegemea zao moja tu la Uchumi la akARAFUU.



Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko katika harakati za kuimarisha miundombinu ili kuyawezesha Makampuni ya Kigeni kupata fursa ya kuwekeza Zanzibar. Alisema wawekezaji katika Sekta ya Utalii wana nafasi nzuri ya uwekezaji kwa vile miundo mbinu ya bara bara, maji na umeme iko katika hatua nzuri.



Hata hivyo Balozi Seif ameuomba Uongozi wa OPIC kuangalia uwezekano wa kuanzisha mradi wa pamoja wa umeme kwa kutumia Nishati ya jua au Bahari ili Zanzibar iwe tayari kukabiliana na upungufu wa huduma ya umeme hasa wakati kinapopungua kina cha maji huko Tanzania Bara.



“ Tumekuwa tukipokea huduma ya umeme kupitia Gridi ya Taifa huko Tanzania Bara, lakini wakati mwengine tunalazimika kupata umeme wa mgao kutokana na kupungua kwa kina cha maji. Hali hii huathiri utendaji kazi na kupunguza kasi ya Maendeleo ya Kiuchumi ”. Alisema Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar. Balozi Seif.