Staa wa Bendi hiyo, Charles Gabriel ‘Chalz Baba’ (wa pili kutoka kulia), akiongoza msafara wa wenzake wakati wa kutoka uwanjani hapo.
Luiza Mbutu (wa pili kulia), akiongelea safari hiyo ilivyokuwa.

Mkurugenzi wa bendi hiyo, Asha Baraka (katikati), akizungumzia ujio wa wanamuziki wake.

BENDI ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’ mapema leo imerejea Bongo ikitokea nchini Uingereza walikokwenda kwa ajili ya ziara ya kimuziki.

Akizungumza na mtandao huu baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, kiongozi wa bendi hiyo, Luiza Mbutu, alisema kuwa wamefarijika na mapokezi waliyopata Uingereza ambapo Balozi wa Tanzania nchini humo na Watanzania waishio huko waliwapa sapoti ya kutosha hadi siku wanarudi.

“Tumefanya kazi yetu vizuri na nina ukakika tumewafurahisha vya kutosha kwani hadi tunaaga kurudi wengi wao walitaka tuendelee kutoa burudani japo hata siku moja zaidi,” alisema Luiza.

( Na GPL.)