PICHA inayodaiwa ni ya staa mmoja wa Bongo akiwa mgongo wazi, imezua utata mitandaoni kutokana na kuchorowa picha ya mkuu wa Freemasons, Lucifa huku watoa maoni wakiwa wanaotea jina la staa huyo bila ya mafanikio.

Wengi wa wadau waliotumbukiza maoni yao, waliandika jina kulingana na macho yao juu ya picha hiyo.
“Huyu hakuna ubishi, ni Wema Sepetu,” aliandika mdau mmoja akisisitiza kuwa, picha hiyo ilipigwa kipindi ambacho Wema alikuwa mpenzi wa kijana mwanamitindo wa Bongo, Jumbe Yusuf Jumbe.

“Hamna, umechemsha. Huyu ni Nelly Kamwelu (Miss Universe 2011, pichani), tena hapo alikuwa chumbani kwake,” aliandika mwingine.

“Nyie wote mnaotea tu, hakuna mwenye uhakika. Huyu ni msanii wa Bongo, Shilole (Zuwena Mohamed),” aliandika mwingine.


 

 “Mm! hakuna haki ya kuandika kama hujafanya utafiti, huyu mrembo mwenye mchoro huu ni msanii mchanga wa filamu za Bongo, Irene Paul, nimewahi kuuona mgongo wake una chata hiyo ya Freemasons,” aliandika mwingine.

Hata hivyo, mastaa hao waliodaiwa ni wahusika wa picha hiyo, walipopatikana kwa njia ya simu walikanusha kuhusika.
Wema: Jamani, hiyo picha si yangu. Sijaiona lakini kwa maelezo hayo kwamba ina mchoro wa Freemasons, si mimi.

Irene: Akha! Toka lini mi nikawa na mchoro wa Freemasons?
Shilole: Mh! Hiyo kali, mi na Freemasons wapi na wapi jamani.

Nelly hakupatikana kuzungumzia madai hayo.
Amani linafanya utafiti wa kina ili kumpata mhusika wa picha hiyo kati ya mastaa wa Bongo.