Mwanamke mtangazaji aliyetokea kumudu sana kutangaza soka Halima Mchuka (Picha juu)amefariki dunia leo alfajiri baada ya kupata tatizo la kiharusi jana akiwa kazini.

Ikitangaza chanzo cha kifo cha Mtangazaji huyo  TBC ilisema kwamba mdada huyo alianguka jana ofisini na kukimbizwa hospitalini ambako alizidiwa na kufariki majira ya saa tisa alfajiri.
“Alikuwa na tatizo hilo jana mchana mara baada ya kutangaza kipindi cha salaam cha TBC-Taifa na akazidiwa ndipo alipopelekwa Hospitali na sasa ndiyo amefariki dunia.”.
Halima Mchuka alijiunga na Radio Tanzania Dar es Salaam miaka ya 1990 na kuondokea kuwa maarufu katika michezo hasa utangazaji wa mpira uwanjani.Tutawaletea habari zaidi hapo baadae. ``Rest in Peace Halima``