Uncleeeee kushoto akiwa na Sharobizo wa Holland Chula wakiwa pamoja kushuhudia wenyewe bila kusimuliwa na mtu kwenye show ya malkia wa mipasho bi Hadija Kopa jijini Den Haag.
Gentlemens wakiwa wamepozi bila wasiwasi nao wakishuhudia burudani ya mkesha wa Christmass toka kwa bi Hadija Omar Kopa.
Nani anasema wanaume hawapendezi? na hawa je?Hongereni kaka zangu mlipendeza sana.
Kinadada watanashati wakiwa na nyuso nzuri huku wakimkodolea macho Malkia Kopa wakati anaendelea kutoa burdani ukumbini hapo.
Malkia wa mipasho ukanda wa Afrika mashariki akiwa na bidada,Mc Seki wakipata Radi ya Camera.
Hii ni zawadi yangu ya Christmass kwa Mr & Mrs Khatib,anayebisha kama hawajapendeza anywe sumu tumuone.
 Raha ya ukumbini pale kila mmoja alikuwa Happy,ebu jionee mwenyewe uongo?
 Malkia wa mipasho akiwa ameketi kwa mapumziko ya muda baada ya kuwachengua na kuchenguka mashabiki wake,Angalia vizuri mkononi mwa Hadija kopa akiwa amekifinyanga vizuri kitita alichotunzwa na mashabiki wake kwa kazi nzuri.Hongera sana Hadija Kopa kwa kazi nzuri Ukumbini pale,kwa kweli kila mmoja ameondoka ametosheka na show yako.
Kutoka kushoto ni mdau ambaye alikuwa ukumbini kupata burdani,mwenye shati la kijani na kizibao cheusi ni Brother Mega akiwa na anayempikia na kumpakulia (mamsapu wake) wakiwa na nyuso za furaha kwa kupata burdani safi toka kwa Hadija Kopa.
Wacha weee,wakati Kopa akiendelea kutoa sauti tamu kwa mashabiki wake,huku nao wakiendeleza mzunguko wa mitikisiko ya pwani.
Ni baba na mama Samantha,kama hukuwepo ukumbini umekosa cha kuhadithia...
Waaww..!!! Mc shupavu Sexy Mama akiwa amepozi kupata radi ya Camera toka kwa mwana Blog wenu,kushoto kwa Sexy Mama ni bidada mtanashati na mpole machoni dada yangu Mariam nae akiwa ametulia vyema kabisa ili kupata burdani toka kwa bi Hadija Kopa.