PICHA ‘mbichi’ zinazomwanika rais wa Shindano la Miss Utalii Bongo, Gideoni Chipungahelo ‘Chipsi’ akiwa na mrembo wake ambaye ni mshiriki wa kinyang’anyiro hicho ngazi ya vyuo vikuu 2011 kwa Mkoa wa Dodoma, Irene Richard wakiwa kitandani, zimenaswa live mtandaoni, Ijumaa lina mikoba kamili.

Picha hizo zinazowaonesha wawili hao wakiwa kihasarahasara chumbani katika uwanja wa kuvutia usingizi, zilianza kusambaa mwanzoni mwa wiki hii ambapo gazeti hili ‘lilifowadiwa’ na chanzo chake.

IJUMAA MZIGONI
Baada ya kuzitia kibindoni, The Udaku Master, Ijumaa lilianza kupepeta ili kupata undani wa ishu hiyo ambapo lilimtafuta mhusika namba moja (Chipsi) ambapo alitoa utetezi wake:

ETI NI PICHA ZA TANGAZO!
“Zilikuwa picha za tangazo la hoteli hiyo kwa ajili ya ‘kuipromoti’ kwa kuonesha mandhari yake.
“Siyo Irene pekee aliyekuwa anahusika, kulikuwa na warembo wengine zaidi ya sita. Hapo nilikuwa nampa mambo mawili matatu juu ya namna ya kupozi ili kupata picha nzuri za mauzo.

“Najua chanzo cha kusambaa kwa picha hizo ni Shaban ambaye alikuwa mmoja wa wanakamati wa Miss Utalii na pia ni mpigapicha wetu. 

NI KISASI?
“Aliahidi kufanya hivyo baada ya kumpiga chini kutokana na utovu wa nidhamu aliouonesha na barua ya kumfukuza kazi nimewatumia mtandaoni.”
Chipsi aliendelea kumtupia mawe Shaban kuwa alilenga kumchafua kabla ya fainali ya kinyang’anyiro hicho kinachotarajiwa kuchukua nafasi Desemba 9, mwaka huu katika Ukumbi wa Royal Village mkoani Dodoma.

HUYU HAPA SHABAN
Katika maelezo yake, Shaban alidai kuwa ana ushahidi wa kutosha juu ya maovu ya Chipsi na yuko tayari kuutoa popote utakapohitajika.