Mama mkazi wa Jangwani, Dar es Salaam eneo lililokumbwa na mafuriko hivi karibuni, akiwa na huzuni baada ya nyumba yake kuwekwa alama ya kubomolewa na wakati wa mchakato wa kuhakiki nyumba hizo uliokuwa unafanywa na Maofisa wa Manispaa ya Ilala.
Mkazi wa Jangwani bondeni, Dar es Salaam, Mohamed Zuberi akilalamika mbele ya wanahabari jana, kuhusu utaratibu unaotumiwa na maofisa wa Manispaa ya Ilala kuhakiki nyumba zao zitakazobomolewa kufuatia amri ya Serikali.
Mkazi wa Jangwani, Dotto Ngoyeji akieleza malalamiko yake mbele ya wanahabari, kwamba Serikali inatakiwa kufuata utaratibu wa kuwatendea haki katika mchakato huo wa kuhakiki nyumba zao.(PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA)