Na Musa Mateja
STAA wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel (pichani) amekwaa skendo ya kupora mume wa Mnenguaji wa Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’, Fasha Joshua, Amani linashikilia mkoba wa tuhuma hizo.
Habari za moto kutoka kwa chanzo chetu, zinasema kuwa, licha ya kudaiwa kupora mwanaume huyo mwenye asili ya Kiarabu na kusababisha mfarakano mkubwa, pia Fasha amenyang’anywa gari aina ya Toyota Cresta namba T 895 BHG na kupewa Aunt.
“Ujue mume wa Fasha, (jina tunalihifadhi kwa sasa) anaishi Dubai, alipokuja Bongo hivi karibuni inadaiwa alikutana na Aunt na kutoka naye. Huyu Aunt sasa amekuwa zoazoa. Awali walianzia kuchati kwenye Facebook baadaye wakakutana live.

“Alipokuja Dar, Aunt akamganda hadi ikafikia hatua jamaa akamuona Fasha si mali kitu, akamnyang’anya gari alilomnunulia na kumpa Aunt ambapo sasa anatanua nalo mitaani,” chanzo kilisema bila kigugumizi.

Kikaendelea: “Siku chache baada ya jamaa huyo kuondoka Bongo, Aunt naye alisafiri kwenda Dubai anapofanyia kazi jamaa na huko ndipo walipomaliza kila kitu. Aunt alipewa kadi ya gari maana alipolinunua, kadi alibaki nayo, gari akampa Fasha.”

Chanzo kikazidi kusema: “Hapa ninapoongea na wewe, ukikutana na Aunt yuko na hilo gari, hasikii cha mtu, ukimuuliza kwa nini amemchukua bwana wa mwenzake, anajibu hajampora, kama ni gari alikabidhiwa na ndugu wa mwanaume hivyo yeye hahusiki na chochote.”

FASHA ANASEMAJE?


Kwa upande wake, mnenguaji huyo alisema anaamini Aunt amempora mwanaume wake, ndiyo maana alinyang’anywa gari na kupewa yeye.
Akasema, mbaya zaidi hata kwenye nyumba aliyokuwa akiishi (kwa wakwe zake), Mwananyamala- Komakoma aliondoka na kuhamia kwa dada yake, Kinondoni- Mkwajuni, Dar.

AUNT NA AMANI HEWANI
Gazeti hili lilimtwangia simu Aunt na kumsomea mashitaka yake ambapo naye bila kusita, alifunguka hivi: “Hayo yote yanayosemwa ni uzushi mtupu, sijapora mume wa mtu na wala sina mpango huo.”

Amani: Mbona inadaiwa licha ya kumchukua mume wa mwenzako, pia umesababisha ameporwa gari na kupewa wewe?
Aunt: Hilo gari nimeuziwa na huyo bwana wa Fasha na ndiyo maana niko nalo, sijapewa bure. Hakuna ukweli mwingine utakaoupata zaidi ya maneno yangu, labda umtafute huyo Fasha naamini atakuwa anafahamu wazi kuwa hilo gari nimeuziwa na hakuna mambo nyuma ya pazia.

Iweje nihongwe gari la Fasha wakati nafahamu alikuwa akilitumia? Huo ni uzushi tu, hauna ukweli hata kidogo.
  
                                        CHANZO CHA HABARI NI GPL