ZIKIWA zimekatika siku kadhaa tangu mwanamuziki Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ (pichani) alazwe nchini Ufaransa akisumbuliwa na ugonjwa aliouita wa ‘heri’, tumbo lake limeonekana kuwa kubwa zaidi na kufanya minong’ono kwamba tayari ni mjamzito. Amani limekuwa likifuatilia kwa karibu afya ya mwanamuziki huyo ambaye ni mke wa aliyekuwa mtangazaji wa Clouds FM, Gardner G.
Habbash na hivi karibuni kwenye ‘blog’ yake alitundika picha ikimuonesha ametinga nguo nyeupe huku tumbo lake likiwa ndii.

Picha hiyo ilizua gumzo kwa mashabiki wake huku wengi wakishadadia kwa kusema lazima litakuwa tumbo la mimba.

Mwenyewe anasemaje?
Sambamba na picha hiyo, Jide aliandika maneno ya mafumbo kwa lugha ya Kiswahili, Kifaransa na Kiingereza akieleza kuwa picha hiyo aliipiga Novemba 1, mwaka huu, lakini hakufafanua zaidi.

Aidha, Jide hakuzungumza chochote kuhusu muonekano wake huo, lakini akaandika maneno yasemayo: ‘Behind the scene part 1’ (nyuma ya pazia sehemu ya kwanza) bila kufafanua.

Wadau wanasemaje?
Kufuatia picha hiyo, baadhi ya wadau waliotembelea mtandao huo walimmiminia pongezi Jide wakiamini kilichomo ndani ya tumbo lake ni mtoto.
Ngaizaskids alisema: “Waooo my luv, jamani nimefurahije nawe mpendwa? Karibu katika ulimwengu huu uliojaa furaha ya aina yake, Mungu awe nawe katika safari nzima…”

Mwingine aliandika: “Yap Komando wangu, ndiyo maana nakupenda sana. Nimefurahi sana dada Jide kwa hiyo hali yako. Hongereni sana, Mungu azidi kukuangalia katika hali hiyo ili tupate anti yetu. Mungu akujalie Mama Kapiteeiiiiiini mtajarajiwa.”

Huyu naye akasema:
“Sasa wale mliokuwa mnasema ….mtanunaje? Mungu ni mwema na hashindwi. TK ana mtoto sasa na Jide soon atapakata wa kwake. Kweli ombea adui yako aishi ili ukifanikiwa ajionee mwenyewe!!!”Je ni ujauzito?
Mwezi Septemba, mwaka huu, Jide alitangaza azma yake ya kutaka kupungaza kitumbo kwa kufanya ‘dayati’ na alifanikiwa katika hilo.

Hata hivyo, siku chache baadaye staa huyo anayemiliki Machozi Band alianza kutokwa na kitumbo cha kiaina, jambo lililozua furaha kwa mashabiki wake.

Yeye amshukuru Mungu
Mara kwa mara Lady Jaydee amekuwa akitundika kwenye mtandao wake maneno ya kumshukuru Mungu kwa yale ambayo amekuwa akimtendea kila siku.
“Mungu ni mkuu, amenitendea makuu…. Sikukata tamaa kama wengine,” alisema Jide ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa akivaa nguo nyeupe bila kuweka wazi sababu ya kufanya hivyo.