Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi mwenge wa uhuru mkuu wa majeshi Jenerali Davies Mwamunyange ambaye atawakabidhi wapandishaji mlima kilimanjaro.
Rais Jakaya Kikwete akiwatakia heri Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Jenerali Davies Mwamunyange na wanajeshi wataopandisha kilele cha mlima Kilimanjaro Mwenge wa Uhuru mkesha wa siku ya uhuru. Kushoto ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Emmanuel Nchimbi , wa pili kulia ni Naibu waziri katika wizara hiyo Dkt Fenella Mukangara na wa kwanza kushoto ni mmoja wa wataopandisha Mwenge mlima Kilimanjaro. (PICHA NA IKULU)
Rais Jakaya Kikwete akihutubia katika maadhimisho ya kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru leo Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam. Walioketi toka kulia ni IGP Saidi Mwema, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange, Spika wa Bunge Mh Anne Makinda
Viongozi wa wataopandisha mwenge wa Uhuru mlima kilimanjaro
Mama Maria Nyerere na Mama Salma Kikwete na wageni wengine mashuhuri jukwaa kuu.