Pichani kushoto Santa Claus akishuka kwenye gari tayari kusalimiana na watoto ili ajumuike nao kwenye sherehe kwa siku ya leo.
Mzungu aliyejipakaza rangi nyeusi usoni kama ishara ya mtu mweusi enzi hizoo ambapo watu weusi walikuwa wakiambatana na Santa Claus kwa kumsaidia kugawa zawadi kwa watu wenye shida.
Wanafunzi wa chekechea na wanafunzi wa shule ya msingi wakiwa tayari kumsikiliza nini Santa Claus anasema.
Santa Claus akiwaeleza mawili matatu watoto ambao walikuwa makini kumsikiliza na kusubiria zawadi zao.
Baada ya kuwapa mawili matatu wanafunzi hao,Santa Claus alitembelea watoto wa majumbani kwenye baadhi ya mitaa jiji Den Haag.
Mmoja wa wadau wakubwa wa Maganga One Blog ni huyu binti,ambaye pia alishiriki katika kumkaribisha Santa Claus alipofika Den Haag leo hii,Kila mtoto alipewa zawadi kama kawaida ya Santa Claus kuwapa watoto zawadi,pichani bidada Laila akiwa ameshikilia zawadi yake mkononi na kofia kubwa.(Picha na maelezo toka kwa Hija wa Maganga One Blog-Den Haag).